JangaAmerika ya Kaskazini
Idadi ya vifo kufuatia mafuriko huko Texas yafikia 119
10 Julai 2025Matangazo
Hata hivyo wasiwasi umezidi kuongezeka kwamba idadi hiyo inaweza kuongezeka maradufu kwa kuwa hadi sasa zaidi ya watu 160 bado hawajulikani walipo.
Maafisa zaidi ya 2,000 wa vikosi vya uokoaji, polisi na wataalam wengine wanaendelea kuwatafuta manusura kufuatia mafuriko ya Julai 4 huku Gavana wa Texas Greg Abbott akiamuru bendera kupepea nusu mlingoti kutokana na janga hilo.
Trump aliyesema kuwa ametuma helikopta kadhaa kwa ajili ya uokoaji, anatarajiwa kuzuru Texas siku ya Ijumaa akiambatana na mkewe Melania Trump.