Idadi ya vifo kufuatia mlipuko Iran imeongezeka hadi 25
27 Aprili 2025Hayo yameripotiwa leo na vyombo vya habari vya serikali wakati kikosi cha wazima moto kikiendelea na juhudi za kuuzima moto huo.
Mlipuko huo wa jana, ambao maafisa wanasema huenda ulisababishwa na vifaa vya kemikali, ulitokea katika sehemu ya Shahid Rajaee ya bandari hiyo, kitovu kikubwa zaidi cha kuhifadhi makontena nchini Iran.
Soma pia: Iran yapendekeza mazungumzo ya nyuklia na nchi za Ulaya
Shirika la kudhibiti majanga limeeleza kuwa kati ya watu 752 waliotibiwa kutokana na majeraha waliyoyapata wakati wa mkasa huo, 190 bado wanaendelea kuhudumiwa katika vituo vya afya.
Waziri wa mambo ya ndani Eskandar Momeni aliyetembelea eneo la mkasa, ameiambia televisheni ya serikali kwamba asilimia 80 ya moto ulikuwa umeshazimwa kufikia Jumapili asubuhi.
Baadhi ya shughuli zimeanza tena katika maeneo ya Shahid Rajaee ambayo hayakuathiriwa na moto au kuharibiwa.