MigogoroMamlaka ya Palestina
ICRC yasema operesheni ya Israel Gaza "sio ya kuvumilika"
21 Agosti 2025Matangazo
Msemaji mkuu wa ICRC, Christian Cardon ameeleza kwamba kuongezeka kwa mapigano Gaza kutasababisha vifo zaidi vya raia, uharibifu wa miundombinu na kuwaacha maelfu ya wengine bila makaazi.
Mpango wa oparesheni mpya ya jeshi la Israel unaojumuisha kuwaita askari wa akiba 60,000, umeongeza hofu ya kuzidisha janga la kibinadamu ambalo tayari ni baya zaidi katika Ukanda wa Gaza.
Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu ina jukumu muhimu Gaza, kando na kutoa misaada ya binadamu, inahusika pia kuratibu na kusimamia ubadilishanaji wa mateka wa Israel wanaoshikiliwa na Hamas.