ICJ yachukuwa jukumu dhidi ya ongezeko la joto duniani
21 Julai 2025Andrew Raine, naibu mkurugenzi wa kitengo cha sheria cha Mpango wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa, amesema kujivuta kwa kasi ya hatua za hali ya hewa kumechochea watu, mashirika na nchi kugeukia mahakama.
Mkutano wa mazingira Paris waingia wiki muhimu ya mwisho
Raine ameiambia AFP kwamba mifumo ya kisiasa inaposhindwa kuchukuwa hatua, sheria inazidi kuonekana kama chombo cha kushinikiza kutekelezwa kwa ahadi ambazo tayari zimeshatolewa.
Jitihada za kupunguza joto ulimwenguni
Hata hivyo amesema ingawa maoni ya ushauri kama ya mahakama ya ICJ hayalazimishwi kisheria, yana umuhimu mkubwa.
Ameendelea kueleza kuwa maoni hayo yanafafanua jinsi sheria ya kimataifa inavyotumika kwa mzozo wa hali ya hewa, hatua inayoziathiri mahakama za kitaifa, michakato ya sheria na mijadala ya umma.