ICC kuomba waranti wa kukamatwa waliohusika na ukatili Sudan
28 Januari 2025Katika eneo hilo kumeripotiwa mauaji ya kikabila yanayofanywa na wanamgambo wa RSF wanaopambana na vikosi vya serikali kwa miezi 19 sasa.
Karim Khan ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa uhalifu unafanyika kila siku huko Darfur na unatumiwa kama silaha ya vita, akisisitiza kuwa ofisi yake imefanya uchunguzi wa kina kwa kuzingatia ushahidi na taarifa muhimu.
Soma pia:Mwendesha mashtaka wa ICC aomba hati za kukamatwa watuhumiwa wa ukatili huko Darfur
Miongo miwili iliyopita, eneo la Darfur lilikumbwa na mauaji ya halaiki na uhalifu wa kivita, yaliyoendeshwa na wanamgambo wa kiarabu wa Janjaweed dhidi ya watu waliojinasibu kama watu wa Afrika Mashariki na Kati.
Karibu watu 300,000 waliuawa na wengine milioni 2.7 walililazimika kuyahama makazi yao.