IAEA: Iran iliongeza akiba yake ya urani kwa kuunda bomu
4 Septemba 2025Matangazo
Hatua ambayo ilikaribia kiwango cha kutengeneza silaha kabla ya Israel kuanzisha shambulio lake la kijeshi mnamo Juni 13. Ripoti ya Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki lenye makao yake Vienna inaeleza kuwa kufikia tarehe 13 Juni, Iran ilikuwa na kilo 440.9 (sawa na pauni 972) za uranium iliyoboreshwa hadi kiwango cha asilimia 60, ikiwa ni ongezeko la kilo 32.3 (sawa na pauni 71.2) tangu ripoti ya mwisho ya IAEA mwezi Mei. Ripoti ya siri pia ilisema kuwa Iran na IAEA bado hawajafikia makubaliano ya kuanza tena ukaguzi wa maeneo yaliyoathiriwa na mashambulizi ya mabomu ya Israel na Marekani mwezi Juni.