HRW: Sudan Kusini ilitumia silaha za moto kuwauwa watu 60
10 Aprili 2025Matangazo
Human Rights Watch, imesema waliohojiwa walitaja matumizi ya silaha za moto zilizoboreshwa katika mashambulizi manne kwenye kaunti za Nasir, Longechuk, and Ulang, pamoja na jimbo la Upper Nile, yaliosababisha mauaji ya watu wapatao 58 na kuwajeruhi vibaya wengine.
Hiki ndicho kitasababisha mvutano mpya Sudan Kusini
Kwa mujibu wa shirika hilo, matumizi ya serikali ya silaha hizo katika maeneo yenye idadi kubwa ya watu yanaweza kuwa uhalifu wa kivita.
Pia imetoa wito kwa Umoja wa Mataifa kutoa wito kwa serikali ya Sudan Kusini kusitisha mashambulizi hayo haramu.
Hata hivyo, serikali haijazungumzia madai hayo.