HRW: Mzozo wa Kongo unaweza kuwa 'janga'
26 Januari 2025Mtafii mkuu wa shirika la HRW barani Afrika Clementine de Montjoye, amesema mahitaji ya kibinadamu yanayohitajika ni makubwa, vinginevyo matokeo mabaya yanaweza kuwafika watu wa eneo la mashariki mwa Kongo.
Soma zaidi: Walinda amani 9 wa Afrika Kusini wameuwawa katika mashambulizi ya waasi DRC
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat ametoa wito wa kusitishwa mara moja mapigano na amezitaka pande zinazohusika kulinda usalama wa raia.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeitisha kikao cha dharura kujadili hali ya nchini Kongo baada ya Kinshasa kuwaondoa wanadiplomasia wake kutoka nchini Rwanda, hatua iliyojibiwa na Rwanda kwa kuwaamuru wanadiplomasia wake kurejea nyumbani kutoka nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.