Watu 7 wauwawa katika shambulio dhidi ya hospitali S.Kusini
3 Mei 2025Matangazo
Watu wengine 20 wamejeruhiwa katika tukio hilo. Shambulio hilo limejiri siku moja baada ya mkuu wa jeshi Paul Majok Nang kutishia kufanya mashambulizi Fangak na katika kaunti nyingine kutokana na boti na majahazi kadhaa kutekwa.
Soma zaidi: MSF yaeleza wasiwasi kuhusu hali nchini Sudan Kusini
Taarifa ya jeshi imewatuhumu wanachama wa vikosi vya makamu wa Rais, Riek Machar na washirika wake wanaojiita White Army kutoka kabila lake la Nuer, kwa kufanya utekaji huo. Hali hiyo inasababisha abiria na wafanyakazi wa vyombo hivyo kushikiliwa mateka huku watekaji wakidai fedha ili wawaachilie huru.