Wakati mapigano yakisimamishwa kati ya jeshi na kundi la waasi la M23 ili kupisha misaada na huduma za kiutu kwa raia nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, hospitali zimehelemewa na idadi kubwa ya majeruhi wa vita, huku kunashuhudiwa uhaba wa dawa na wahudumu wa afya.