Hofu ya kujifungua ni hali inayowakumba wanawake wengi hasa wale wanaojifungua kwa mara ya kwanza. Wanawake hupata mchanganyiko wa wasiwasi wa kimwili, kihisia na kiakili unaotokana na matarajio ya maumivu, hatari za kiafya au hadithi za kutisha kutoka kwa wanawake wengine waliowahi kujifungua. Veronica Natalis anaangazia kadhia hiyo katika Makala ya Afya Yako.