HO CHI MIN CITY:Kimbunga damrey hadi sasa kimeshasabisha watu 45 kuuawa.
28 Septemba 2005Matangazo
Hadi sasa idadi ya watu waliokwishatambulika wamekufa kutokana kimbunga Damrey,kilichopiga maeneo ya kusini-mashariki mwa Asia imefikia 45.
Katika siku chache zilizopita,kimbunga hicho kilipita maeneo ya kisiwa kikubwa cha Philippine cha Luzon,kisiwa cha Hainan kusini mwa China,Vietnam,Laos na kaskazini mwa Thailand.
Maofisa wa China na Vietnman wamesema kimbunga Damrey,ni moja ya vimbunga vikubwa kuwahi kupiga maeneo hayo kwa miaka kadhaa sasa,ambapo kimeharibu nyumba,kukata nyaya za umeme na halikadhalika kimevuruga mazao ya kilimo mashambani.
Kimbunga hicho kwa sasa kimepungua kasi yake baada ya kupiga nchini Vietnam.Maelfu ya watu wamelazimika kuyahama makazi yao.