TeknolojiaUingereza
Hitilafu ya umeme yatatiza safari uwanja mkubwa wa Heathrow
21 Machi 2025Matangazo
Safari za mamia kwa maelfu ya abiria duniani zimetatizika baada ya ndege kushindwa kuruka au kutua kwenye uwanja huo tangu mapema leo alfajiri.
Mtandao wa kufuatilia safari za ndege wa FlightRadar umesema karibu ndege 1,350 zimeathirika na hitilafu iliyotokea.
Soma pia:Mgomo mkubwa wa viwanja ndege waendelea Ujerumani
Mashirika kadhaa yamelazimika kuwapeleka abiria waliotarajiwa kuwasili au kuunganisha safari kupitia Heathrow kwenye viwanja vingine vya ndege barani Ulaya.
Mamlaka za uwanja huo zimesema bado hazifahamu muda ambao umeme utarejea, maelezo yanayozidisha mashaka kuwa mparaganyiko wa safari utaendelea kwa muda mrefu kuliko ilivyotarajiwa.