SiasaLebanon
Hezbollah yawataka mawaziri wa Lebanon kutumia hekima
6 Septemba 2025Matangazo
Kundi la Hezbollah nchini Lebanon limeyasema hayo kutokana nampango wa serikali wa kutaka kuwanyang'anya silaha wapiganaji wa Hezbollah.
Afisa wa Hezbollah Mahmoud Qmati, amesema kundi hilo linazingatia kikao cha baraza la mawaziri cha siku ya Ijumaa kuhusu mpango wa jeshi wa kulipokonya kundi lake silaha kwa kutahadharisha kuwa jeshi la Lebanon halina uwezo mkubwa na hivyo kuendelea kwa operesheni za kijeshi za Israel nchini humo kutazidi kulikwamisha jeshi lenye uwezo mdogo.
Hata hivyo baraza la mawaziri la Lebanon limeuunga mkono mpango huo na limesema jeshi litaanza kuutekeleza, ingawa muda wa kuanza utekelezaji wake haujawekwa wazi.