Heusgen: Mkutano wa Usalama wa Munich "jinamizi kwa Ulaya"
17 Februari 2025Matangazo
Christoph Heusgen amaitoa kauli hiyo Jumapili baada ya kuhitimisha mkutano huo uliyowaleta pamoja viongozi wa dunia na wataalamu wa sera za kigeni.
Walakini, Heusgen ameongeza kuwa mkutano huo hata hivyo umewezesha kuyaweka bayana mambo muhimu, akisisitiza kuwa Marekani chini ya utawala wa Trump ni kama inaishi kwenye sayari nyingine.
Soma pia: Mkutano wa usalama mjini Munich waingia siku yake ya mwisho
Heusgen ameyasema hayo kufuatia mivutano kadhaa kati ya Marekani na Ulaya iliyoshuhudiwa kwenye mkutano huo wa Usalama wa Munich, kuanzia kauli za Makamu wa rais wa Marekani JD Vance akiwashutumu washirika wa Ulaya kwa kuhatarisha demokrasia, na wazo la kuitenga Ulaya kwenye mazungumzo ya amani kuhusu Ukraine.