MigogoroAfrika
Helikopta ya Umoja wa Mataifa yashambuliwa Sudan Kusini
8 Machi 2025Matangazo
Taarifa hizo zimetolewa na ofisi ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo UNMISS. Inaarifiwa wanajeshi kadhaa wa jeshi la Sudan Kusini ni miongoni mwa waliouawa huku Jenerali mmoja amejeruhiwa.
Wanajeshi hao ilikuwa wahamishwe na ujumbe wa UNMISS kutoka mji wa Nasir, ambao unawaniwa kati ya serikali na kundi la wanamgambo wa kabila la Nuer ambalo ni asili ya makamu wa Rais wa nchi hiyo Riek Machar. Serikali inakilaumu chama cha Machar cha SPLM-IO kuchochea mzozo huo.
Kulingana na Umoja wa Mataifa mapigano hayo kwenye mji wa Nasir, ulio karibu na mpaka wa Ethiopia yamewaua watu kadhaa na kuwalazimisha wengine kuyakambia makao yao.