HELIKOPTA YA MAREKANI YAANGUSHWA IRAQ:
14 Januari 2004Matangazo
BAGHDAD: Wanamgambo nchini Iraq wameiangusha helikopta ya jeshi la Kimarekani,hii ikiwa ni mara ya tatu katika kipindi cha wiki mbili.Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la Kimarekani shambulio hilo limetokea karibu ya mji wa Fallujah.Akaongezea kuwa wanajeshi 2 waliokuwemo ndani ya helikopta hiyo aina ya Apache wamenusurika.Kwa upande mwingine ripoti zinasema watu 3 wameuawa mjini Fallujah,baada ya wanajeshi wa Kimarekani kukifyetulia risasi kikundi cha wafanya maandamano.Stesheni ya televisheni ya kiarabu Al Jazeera imeripoti kuwa waandamanaji walikuwa wakidai mwanamke aliewekwa kizuizini akishukiwa kuhusika na vitendo vya kigaidi aachiliwe huru.