Helikopa ya Kimarekani yadenguliwa Afghanistan:
22 Februari 2004Matangazo
KANDAHAR: Nchini Afghanistan, helikopa yenye watumishi wa Kimarekani ilishambuliwa na kuangushwa. Msemaji wa Ubalozi wa Marekani mjini Kabulalisema, rubani wa Kiingereza wa helikopa hiyo aliuawa na Mmarekani mmoja kujeruhiwa. Halikopa hiyo ilidenguliwa Kilomita kama 65 Kusini-Magharibi mwa mji wa Kandahar. Helikopta hiyo inamilikiwa na kiwanda cha ujenzi cha Kimarekani linaloandaa harakati za ujenzi wa barabara kuu kati ya mji mkuu wa Afghanistan na Kandahar. Inasemekana njia hiyo haina usalama kwa sababu ya kutokea mashambulio na utekaji nyara wa mara kwa mara kupitia wanamgambo wa Taliban.