HEILIGENDAMM: Rais Bush aendelea na ziara nchini Ujerumani
13 Julai 2006Matangazo
Rais George W. Bush wa Marekani anaendelea na ziara nchini Ujerumani leo anatarajiwa kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Kansela Angela Merkel.
Pamoja na masuala mengine viongozi hao watajadili njia za kuwa na msimamo wa pamoja juu ya mzozo wa nyuklia wa Iran na juu ya jela ya Guantanamo.
Kansela Merkel , ameshatoa miito kadhaa kuitaka Marekani iifunge jela hiyo.
Rais Bush atamaliza ziara yake ya nchini Ujerumani hapo kesho na kuelekea Urusi ambapo atahudhuria mkutano wa nchi nane tajiri duniani utakaofanyika katika mji wa St.Petersburg.