MigogoroMarekani
Marekani yazuia azimio la UN la usitishwaji vita Gaza
5 Juni 2025Matangazo
Mjumbe wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Dorothy Shea amesema azimio hilo litadhoofisha juhudi za kidiplomasia za kufikia usitishaji mapigano unaoakisi uhalisi wa mambo na badala yake litawaongezea hamasa kundi la Hamas.
Ameongeza kuwa azimio hilo halitoi uwiano sawa kati ya Israel na Hamas.
Rasimu ya azimio hilo ilitaka "usitishwa wa mara moja, bila masharti na wa kudumu wa mapigano huko Gaza na hatua hiyo kuheshimiwa na pande zote.