Hatua ya kusitisha ufadhili wa USAID ni kinyume cha katiba
19 Machi 2025Matangazo
Jaji mmoja wa Marekani ameizuia serikali ya Marekani na bilionea Elon Musk kutochukua hatua zaidi za kulifunga Shirika la Kimataifa la Misaada la Marekani USAID, akisema hatua hiyo huenda imekiuka katiba. Katika uamuzi wake wa awali, Jaji Theodore Chuang huko Maryland amemuamrisha mshauri wa Rais Donald Trump, Musk na shirika analoliongoza kuwarejeshea haki za mifumo ya kompyuta wafanyakazi wa kudumu wa shirika hilo na wale walio na mikataba wakiwemo maelfu waliosimamishwa kazi. Uamuzi huo unakuja baada ya kesi zilizowasilishwa mahakamani na wafanyakazi wa sasa na wa zamani wa shirika hilo la misaada.