Harambee Stars yapata ushindi wa 1-0 dhidi ya DR Congo
3 Agosti 2025Matangazo
Mchezaji Austin Odhiambo, kiungo wa Gor Mahia, ndiye aliyeifungia Kenya bao hilo la pekee kunako dakika za mwisho za kipindi cha kwanza.
Kongo ilionekana kuwa na nguvu mwanzoni mwa mchezo huku wakilazimisha makosa kutoka safu ya ulinzi ya Harambee Stars.
Ushindi huu ni mwanzo mzuri kwa Harambee Stars katika kampeni yao ya CHAN na umeongeza matumaini kwa vijana wa Benni McCarthy kufuzu katika hatua ya mtoano.
Rais William Ruto amewaahidi wachezaji wa Harambee Stars shilingi milioni 600 iwapo timu hiyo itachukua ubingwa wa CHAN mwaka huu, pamoja na shilingi milioni moja kwa kila mchezaji kwa kila ushindi wa mechi katika michuano hiyo.