Harambee Stars kuanza kampeni yao ya CHAN dhidi ya DR Kongo
3 Agosti 2025Matangazo
Mechi hiyo ya kundi B itakayochezwa katika uwanja wa Kasarani jijini Nairobi, itakuwa mara ya kwanza kwa mataifa hayo mawili kukutana katika michuano ya CHAN.
Kenya inashiriki michuano ya CHAN kwa mara ya kwanza na ni mwenyeji wa michuano hiyo pamoja na Uganda na Tanzania.
Rais William Ruto ameahidi zawadi ya shilingi milioni 600 kwa Harambee Stars endapo watashinda taji hilo pamoja na marupuru kwa kila ushindi.
Ameongeza kuwa kila mchezaji atatuzwa shilingi milioni moja kwa kila mechi ambayo timu hiyo itapata ushindi katika michuano ya CHAN.