Flick awahimiza wachezaji kuwa tayari kwa "mtihani" wa Inter
30 Aprili 2025Flick ameongeza kuwa Inter Milan ina safu nzuri ya ulinzi na wanashambulia kwa kasi, na hivyo lazima wachezaji wake wawe makini uwanjani.
Barcelona iko katika fomu nzuri kuelekea mechi ya leo hasa baada ya mwishoni mwa wiki kupata ushindi wa 3-2 dhidi ya wapinzani wao Real Madrid katika fainali ya Kombe la Copa del Rey.
Soma pia: Dabi ya Madrid yakosa mvuto
Vijana wa Hansi Flick sasa wanaelekeza nguvu zao katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya ambapo wanapania kushinda taji hilo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2015.
Hata hivyo kwa upande wa Inter Milan, klabu hiyo inayotiwa makali na Simone Inzaghi imepata matokeo mabaya katika wiki za hivi karibuni kwenye Ligi Kuu ya Italia, wakifungwa na AS Roma na Bologna na sasa imeshuka hadi nafasi ya pili nyuma ya Napoli, pamoja na kutolewa nje ya Kombe la Coppa Italia na wapinzani wao AC Milan.