Hamas: Watu 70 wameuwawa Gaza ndani ya saa 24 zilizopita
27 Juni 2025Wizara hiyo imeripoti vifo 72 huku wengine 174 wakijeruhiwa ndani ya saa hizo. Hata hivyo wizara hiyo haijaitenganisha idadi hiyo kufahamu hasa ni raia na wanamgambo wangapi waliouwawa.
Tangu mapigano kuanza mjini Gaza mnamo Oktoba 7 mwaka 2023 zaidi ya watu 56,000 wameuwawa huko, huku zaidi ya 132,000 wakijeruhiwa hii ikiwa ni kwa mujibu wa duru za wapalestina.
Idadi ya Wapalestina waliouwawa kwa mashambulizi ya Israel Ukanda wa Gaza yafika watu 56
Wanajeshi wa Israel wamekuwa wakiwashambulia wanamgambo wa Hamas na makundi mengine ya wanamgambo wa kipalestina tangu Hamas iliposhambulia Kusini mwa Israel Oktoba 7 na kusababisha mauaji ya watu 1,200 na zaidi ya wengine 200 wakichukuliwa mateka na kundi hilo.
Kisa hicho ndio kilichosababisha mgogoro kati ya mahasimu hao wawili unaoshuhudiwa kwa sasa Mashariki ya Kati.