SiasaMamlaka ya Palestina
Hamas yasema imejibu pendekezo la kusitisha mapigano
24 Julai 2025Matangazo
Kundi hilo la wanamgambo wa Kipalestina limesema "limewasilisha majibu yake na ya makundi mengine ya Kipalestina kwa wasuluhishi ambayo yanajumuisha mapendekezo ya kurekebisha vipengele kadhaa hasa kuhusu uingizaji wa misaada, maeneo ambayo jeshi la Israel linapaswa kuondoka, pamoja na kuhakikishiwa makubaliano ya kudumu ya kuvimaliza vita hivyo.
Ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, imethibitisha kupokea majibu ya Hamas na kwamba wanaendelea kuyapitia.
Wajumbe kutoka pande zote mbili wamekuwa wakifanya mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja huko Doha kupitia wasuluhishi, Hata hivyo, mazungumzo yameendelea kwa zaidi ya wiki mbili bila mafanikio, huku kila upande ukilaumu mwingine kwa kushikilia misimamo mikali.