Hamas yasema iko tayari kwa makubaliano ya amani
4 Septemba 2025Matangazo
Taarifa yake hiyo ya jana jioni inasema kundi hilo bado linasubiri majibu kutoka kwa Israel kuhusu pendekezo la hivi karibuni la wapatanishi wa kimataifa kuhusu kusitisha mapigano.Kwa mujibu wa Waziri wa Ulinzi wa Israel, Israel Katz masharti ya taifa lao katika makubaliano hayo ni pamoja na kuachiliwa kwa mateka wote na kuondolewa kwa nguvu za kivita kwa Hamas. Lakini taarifa kutoka ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, ilisema kuwa tangazo la Hamas ni: "propaganda nyingine tu" ambayo haina jipya.