Hamas yasema iko tayari kwa awamu ya pili ya kusitisha vita
3 Februari 2025Matangazo
Hayo yameripotiwa na shirika la habari la AFP likiwanukuu maafisa wawili wa kundi hilo la Wapalestina linalotawala Ukanda wa Gaza. Mmoja wa maafisa hao amesema Hamas iliwaarifu wapatanishi wiki iliyopita kuwa iko tayari kuanza mazungumzo ya awamu ya pili.
Matamshi hayo yametolewa wakati Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu yuko nchi Marekani kwa mkutano na Rais Donald Trump kesho Jumanne ambao yumkini utatawaliwa na suala la vita vya Gaza.
Soma pia:Netanyahu kujadili na Trump "ushindi dhidi ya Hamas"
Hivi sasa Israel na kundi la Hamas wanatekeleza mkataba wa kusitisha mapigano kwa wiki sita ambao umefanikisha kuachiwa huru kwa mateka 18 wa Israel na mamia ya Wapalestina waliokuwa wamefungwa jela.