Hamas yasema iko tayari kuzungumza mara moja
8 Septemba 2025Matangazo
Kundi la Hamas limesema liko tayari kukaa mara moja kwenye meza ya mazungumzo kufuatia kile lilichokieleza kuwa ni mawazo kadhaa kutoka kwa Marekani yanayolenga kuafikiwa kwa mkataba wa kusitisha mapigano.
Kundi hilo la wanamgambo wa kipalestina limesema linakaribisha mpango unaounga mkono juhudi za kufikisha mwisho uvamizi na machafuko dhidi ya raia wake na kuthibitiisha liko tayari kwa mazungumzo kujadili kuachiwa huru kwa wafungwa wote.
Taarifa ya Hamas imekuja baada ya rais wa Marekani Donald Trump kusema alikuwa ametoa onyo la mwisho kwa Hamas kukubali mkataba wa kuwaachia huru mateka katika Ukanda wa Gaza.