Hamas yakubali pendekezo la kusitisha mapigano Gaza
19 Agosti 2025Naim aliandika Jumatatu katika mtandao wa kijamii wa Facebook kuwa kundi hilo limewasilisha jibu lake, lilikubaliana na pendekezo hilo la wapatanishi.
Naim amesema wanamuomba Mwenyezi Mungu avimalize vita hivyo.
Awali chanzo cha Hamas kilisema kuwa kundi hilo limekubali pendekezo bila ya kuomba lifanyiwe marekebisho yoyote.
Misri amesema Qatar ililituma pendekezo hilo jipya kwa Israel. Hata hivyo, Israel bado haijajibu.
Pendekezo hilo linajumuisha kusitisha mapigano kwa muda wa siku 60, kuachiliwa baadhi ya mateka, kuachiliwa huru wafungwa kadhaa wa Kipalestina na kuruhusu misaada kuingizwa Gaza.
Wakati huo huo, meli ya mizigo iliyopakia takribani tani 1,200 za misaada ya Ukanda wa Gaza, imeondoka katika mji wa bandari wa Limassol, nchini Cyprus.
Misaada inayohitajika haraka, itapelekwa kwanza katika bandari ya Israel ya Ashdod.