MigogoroMamlaka ya Palestina
Hamas yakubali kumwachilia huru mateka raia wa Marekani
12 Mei 2025Matangazo
Maafisa wawili wa Hamas wameliambia shirika la Habari la Associated Press kwamba wanatarajia kumuachilia huru mateka huyo katika muda wa saa 48 zijazo.
Mjumbe wa Rais wa Marekani Donald Trump wa eneo la Mashariki ya Kati Steve Witkoff, amethibitisha jana Jumapili kwamba Hamas imekubali kumuachilia Alexander kama ishara ya nia njema kuelekea kwa kiongozi huyo wa Marekani.
Soma pia: Marekani yasema wakfu mpya utapeleka misaada Gaza
Tangazo la kuachiliwa kwa mateka huyo kwa mara ya kwanza tangu Israel ilipokiuka mpango wa usitishaji mapigano mnamo mwezi Machi, limetolewa muda mfupi kabla ya Trump kufanya ziara Mashariki ya Kati wiki hii.