MigogoroMashariki ya Kati
Hamas yaishutumu Israel kuchelewesha kufikishwa msaada Gaza
29 Januari 2025Matangazo
Maafisa wamesema hali hiyo ni kinyume na makubaliano ya kusitisha mapigano na kuonya hatua hiyo inaweza kuathiri mchakato wa kuachiliwa kwa mateka.
Afisa mwingine, aliyezungumza kwa sharti la kutotambulishwa amesema kundi hilo limewaomba wapatanishi wa Misri, mjini Cairo kuingilia kati suala hilo.
Maafisa wa Hamas wamesema Israel ilishindwa kupeleka vifaa muhimu kama mafuta, mahema, mashine na vifaa vingine, kama walivyokubaliana kufanyika katika awamu ya kwanza ya makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyoanza kutekelezwa Januari 19.
Hata hivyo, Israel kupitia shirika linalosimamia mahusiano ya raia, COGAT, imezipuuza shutuma hizo ikisema ni za uongo.