Hamas wahimizwa wakubali mkataba ili misaada iingie Gaza
22 Aprili 2025Matangazo
Balozi wa Marekani nchini Israel Mike Huckabee amelitolea wito kundi la wanamgambo wa kipalestina la Hamas likubali mkataba utakaowezesha kuachiwa huru mateka kwa mabadilishano na kuruhusiwa misaada ya kibinadamu kuingia Gaza.
Ujumbe wa Huckabee alioutoa jana Jumatatu unakuja baada ya Hamas Alhamisi iliyopita kuashiria kulikataa pendekezo la sasa la mkataba wa Israel, ambao duru ya Hamas ilisema unapendekeza mabadilishano ya wafungwa na kuruhusiwa msaada katika Ukanda wa Gaza.
Mpatanishi mkuu wa Hamas amesema kundi hilo linakataa kukubaliana kwa sehemu na linataka mkataba kamili ikiwa ni pamoja na kuvifikisha mwisho vita na Israel iondoke kutoka Gaza.